Thursday, July 16, 2015

Klabu ya Liverpool yaweka paundi milioni 32.5 kwaajili ya kumsajili Christian Benteke


Majogoo wa jiji la Liverpool nchini Unigereza wapo tayari kuweza kutumia kiasi cha paundi milioni 80 kwaaajili ya kufanya usajili wa ligi kuu nchini Uingereza alimaarufa kama EPL, Liverpool ipo tayari kutoa zaidi ya paundi miloni 80 kwaajili ya kununua sehemu ya mkataba wa mshambuliaji wa Aston Villa, Christian Benteke.

Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers amesema kwamba hakuna haja ya kuziba pengo la Raheem Steling


Brendan Rodgers ameliembai gazeti moja nchini Uingereza kuwa klabu yake ya Liverpool haina haja ya kufanya usajili wa winga wakujakuziba nafasi ya Raheem Sterling aliyehamia katika klabu ya Manchester City kwa ada ya paundi milioni 49.5 ambapo imeelezwa kuwa ndiyo usajili mkubwa uliofanyika katika dirisha la usajili la msimu huu.

Manchester United kumuuza Victor Valdes baada ya kukataa kucheza nafasi ya golikipa wa akiba (Reserves)


Golikipa Victor Valdes atauzwa na manchester United baada ya Manager Louis Van Gaal kuthibisha kuwa golikipa Victor Valdes alikataa kucheza nafasi ya golikipa wa akiba katika msimu wa mwaka jana ambao ulimazika kwa Valdes kuwa golikipa wa akiba (Reserve)

Klabu ya Leicester City yaweka imani kwa Esteban Cambiasso kuongeza mkataba mpya


Klabu ya Leicester City imekuwa na tumaini la kumshauri mchezaji Esteban Cambiasso kuongeza mkataba mpya kufuatia uteuzi wa Boss wa zamani wa klabu ya Intermilan, Claudio Ranieri ambaye kwa sasa ameinunua klabu ya Leicester City, Claudio Raniera anamtaka Combiasso kuongeza mkataba wa miaka mitatu katika ya klabu ya Leicester City.

Tuesday, July 7, 2015

Luis Nani ndiyo mchezaji wa kwanza kununuliwa kwa gharama kubwa katika klabu ya Fenerbahce


Mchezaji wa Manchester United, Luis Nani ambaye alisajili na klabu ya Sportin Lisbon  ya nchini Ureno kwa mkopo kabla hajasajiliwa rasmi na klabu ya Fenerbahce. Nani ambaye aliichezea Manchester United kwa takribani misimu mitatu tangu asajiliwe na Manchester United ambayo kipindi hicho ilikuwa chini ya uongozi wa kocha Sir. Alex Furgason  ambaye amesataafu kuwa kocha.


Kevin Prince-Boateng anaweza kusajiliwa na Galatasaray au AC Milan


Wakala wa mchezaji wa kimataifa wa Ghana, Kevin Prince-Boateng  amesema kwamba mshambuliaji wa Schalke 04 ya Ujerumani, Kevin Prince-Boateng anaweza kujiunga na klabu ya Galatasaray au anaweza kurudi katika klabu yake ya zamani ya AC Milan.

Saturday, July 4, 2015

Yanga SC yakubali yaishe baada Kiiza kusajiliwa na Simba SC


Kitendo cha strika Hamis Kiiza "Diego" kusaini mkataba wa kucheza Simba SC kimeweza kuwatetemesha wana wajangwani Yanga SC baada ya nahodha wa Yanga Nadir Haroub "Cannavaro" kukili kuwa Hamis Kiiza ni moja kati ya washambuliaji hatari sana.

Marcos Rojo asema kwamba Angel Di Maria yupo katika kiwango sawa na Messi na Ronaldo


Beki wa Manchester United na timu ya taifa ya Argentina Marcos Rojo amesema kwamba mchezaji mwenzake wa Manchester United na timu ya taifa ya Argentina Angel Di Maria yupo katika kiwango sawa na wachezaji wa dunia ambao ni Lionel Messi na Christian Ronaldo. Marcos Rojo anaamini kuwa Angel Di Maria atakuja kuwa sawa na Messi na Ronaldo katika hadhi ya kimchezo na hata kuwania tuzo ya mchezaji wa bora duniani.

Lukas Podolski asajiliwa na klabu ya Galatasaray


Klabu ya Galatasaray ya nchini Uturuki imethibitisha kuwa wamemsajili mshambuliaji wa Arsenal, Lukas Podolski, Wakala wa Lukas podolski aliliambia gazeti la "Bold" siku ya Ijumaa kwamba mchezaji wa kimataifa wa Ujerumani Lukas Podolski ameamua kuondoka Arsenla baada ya kukosa uhakika wa kuwepo katika kikosi cha kwanza cha kocha Arsen Wenger.

Ajax inatarajia kubaki kwa golikipa Jasper Cillessen.


Klabu ya Ajax imeweka wazi kuwa bado inatarajia kubaki kwa golikipa wao tegemezi Jasper Cillessen licha ya golikipa huyo kutakiwa na klabu ya Manchester United ambayo inamuhitaji mlinda mlango huyo ili kuja kuziba nafasi ya David De Gea ambye ametimkia zake Real Madrid.

Thursday, July 2, 2015

Antonio Rudiger anatakiwa na Chelsea pamoja Wolfsburg


Klabu ya Chelsea na klabu ya Wolfsburg ya Ujerumani vinataka kumsajili beki wa kati wa klabu ya Stuttgart ya nchini Ujerumani, Gazeti la "Bild" liliripoti kuwa Beki huoy wa Stuttgart, Antonio Rudiger ameshakubaliana na klabu ya Wolfsburg katika masharti ya kimkataba na klabu hiyo lakini bado vilabu hivyo viwili vinafanya makubaliano na beki huyo wa Stuttgart huku klabu ya Stuttgart ikitaka ada ya paundi milioni 18 ilikuweza kumuachia Antonio Rudiger.

Rickie Lambert yupo tayari kuondoka Liverpool


Strika wa Liverpool, Rickie Lambert amethibitisha kuwa anatarajia kuondoka Anfield msimu huu, Lambert ambaye alikuwa katika kupambana kuhakikisha anarudisha kiwango chake baada ya usajili wake wa kushtukiza akiwa anatokea Southampton msimu uliopita wakati huo Aston Villa alikiwa ikisikika kumwania straika huyo wa Uingereza.