Saturday, July 4, 2015
Lukas Podolski asajiliwa na klabu ya Galatasaray
Klabu ya Galatasaray ya nchini Uturuki imethibitisha kuwa wamemsajili mshambuliaji wa Arsenal, Lukas Podolski, Wakala wa Lukas podolski aliliambia gazeti la "Bold" siku ya Ijumaa kwamba mchezaji wa kimataifa wa Ujerumani Lukas Podolski ameamua kuondoka Arsenla baada ya kukosa uhakika wa kuwepo katika kikosi cha kwanza cha kocha Arsen Wenger.
Lukas Podolski mwenye umri wa miaka 30 alisajiliwa kwa mkopo na klabu ya Intermilan msimu uliopita, mchezaji huyo kwa sasa amesajiliwa na klabu ya Uturuki na huku klabu ya Galatasaray imethibitisha hilo hii leo na kusema kwamba dili hilo litakamilika siku za hivi karibuni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment