Saturday, July 4, 2015
Marcos Rojo asema kwamba Angel Di Maria yupo katika kiwango sawa na Messi na Ronaldo
Beki wa Manchester United na timu ya taifa ya Argentina Marcos Rojo amesema kwamba mchezaji mwenzake wa Manchester United na timu ya taifa ya Argentina Angel Di Maria yupo katika kiwango sawa na wachezaji wa dunia ambao ni Lionel Messi na Christian Ronaldo. Marcos Rojo anaamini kuwa Angel Di Maria atakuja kuwa sawa na Messi na Ronaldo katika hadhi ya kimchezo na hata kuwania tuzo ya mchezaji wa bora duniani.
Di Maria ambaye alisajilwa na Manchester United kwa ada ya paundi milioni 59.7 akitokea Real Madrid msimu uliopita, huku winga huyo hatari akiripotiwa na uvumi wa kutakiwa na vilabu vya Paris Saint German pamoja na Bayern Munich ambazo zinataka kumsajili Angel Di Maria.
Wakati akifanya mazungumzo na gazeti la Daily Mail Marcos Rojo alisema "Angel Di Maria ni moja kati ya wachezaji bora duniani na anaweza kufanya vitu vizuri kama Messi na Ronaldo" Marcos Rojo aliendelea kwa kusema.
"Watu wamesahau kuwa msimu uliopita Di Maria alikuwa akijaribu kwenda sawa na mazingira ya ligi ya English premier league, watu waliona tu ada kubwa ya uhamisho lakini labda hawakufikiria kwamba ligi ya Uingereza ni ngumu ukitofautisha na ligi ya Hisapania, nadhani ni swala la kuwa fiti uwanjani na nina uhakika msimu ujao tutaona mambo mazuri kutoka kwa Angel Di Maria"
Marcos Rojo aliendelea kwa kumzungumzia kocha Mholanzi Louis Van Gaal kwa kuweza kuiendesha Manchester United kurudi katika hatua ya kutaka ubingwa wa ligi msimu ujao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment