Tuesday, July 7, 2015
Luis Nani ndiyo mchezaji wa kwanza kununuliwa kwa gharama kubwa katika klabu ya Fenerbahce
Mchezaji wa Manchester United, Luis Nani ambaye alisajili na klabu ya Sportin Lisbon ya nchini Ureno kwa mkopo kabla hajasajiliwa rasmi na klabu ya Fenerbahce. Nani ambaye aliichezea Manchester United kwa takribani misimu mitatu tangu asajiliwe na Manchester United ambayo kipindi hicho ilikuwa chini ya uongozi wa kocha Sir. Alex Furgason ambaye amesataafu kuwa kocha.
Luis Nani aliyekuwa akicheza kwa mkopo katika klabu Sporting Lisbon ya Ureno ambapo ameichezea klabu hiyo kwa msimu mmoja na kuweza kusajiliwa na klabu ya nchini Uturuki klabu ya Fenerbahce ambayo ilimsajili Lius Nani kwa ada ya paundi milioni 24 akitokea Manchester United. kutokana na usajili huo ulifanywa na Fenerbahce ndiyo unaoifanya klabu ya Fenerbahce kufanya usajili wa gharama kubwa katika klabu hiyo ya nchini Uturuki.
Baada ya kusajiliwa rasmi na Fenerbahce Luis Nani kwa sasa atakuwa akiitumikia klabu hiyo mpaka pale mkataba wake utakapo malizika na kwenda kutafuta klabu nyingine ya kuichezea.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment