Saturday, July 4, 2015

Ajax inatarajia kubaki kwa golikipa Jasper Cillessen.


Klabu ya Ajax imeweka wazi kuwa bado inatarajia kubaki kwa golikipa wao tegemezi Jasper Cillessen licha ya golikipa huyo kutakiwa na klabu ya Manchester United ambayo inamuhitaji mlinda mlango huyo ili kuja kuziba nafasi ya David De Gea ambye ametimkia zake Real Madrid.


Boss wa klabu ya Ajax, Frank De Boer alisema kwamba anatarajia mlinda mlango Jasper Cillessen ataendelea kubaki Ajax licha yakutaiwa na klabu ya Manchester United, Boss Frank De Boer aliliambia gazeti la "Voetbal International" kwamba ataendelea kmuweka Jasper Cillessen katika klabu ya Ajax na hawatamuuza kwenda klabu yoyote.

Akizungumza na gazeti hilo Boss Frank De Boer alisema, "Jasper Cillessen ni golikipa muhimu kwetu kwahiyo hatutaki kumpoteza" alisema De Boer.

Jasper Cillessen amekuwa chaguo namba moja katika timu ya taifa ya Uholanzi baada ya kocha Mholanzi Luis Van Gaal kuichukua timu hiyo na kuweza kushika nafasi ya tatu katika fainali za kombe la dunia 2014.

No comments:

Post a Comment