Wednesday, June 17, 2015

Sakata la Jerry Muro kutimuliwa Yanga SC.

Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa club ya Yanga SC, Jerry Muro amekanusha taarifa za kutimuliwa kwa kosa la kiutovu wa nidhamu.

Taarifa zilizochapicsha katika gazeti la Uhuru hii leo ambazo zilisema kuwa kiongozi mmoja wa club ya Yanga ambaye hakupenda kutajwa jina lake kwasababu hakua na mamlaka ya kulizungumzia sakata hilo. Kiongozi huyo alisema kuwa Jerry Muro ametimuliwa katika club ya Yanga baada ya kufanya kazi kinyume na maagizo ya uongozi wa club ya Yanga.

Kiongozi huyo alisema kikao cha dharura cha kumfuta Muro katika kazi kilifanyika juzi kabla ya maadhimio kupelekwa kwa mwenyekiti wa club hiyo ambaye ni Yusuph Manji.

Baada ya taarifa hizo Jerry Muro alijibu sakata hilo kwa sema hivi, "Ndugu zangu nimepigiwa simu nyingi sana asubuhi hii nimeona katika gazeti la Uhuru kuhusiana na taarifa zangu za kuondoka Yanga wakati nachukua hatua dhidi ya upotoshaji huu wa habari, naomba niseme jambo moja mimi bado nipo Yanga kama mkuu wa habari na mawasiliano  na mimi bado ni mwanachama hai wa Yanga mwenye kadi namba 028508 nipo Yanga na nitaendelea kuwa Yanga" hivyo ndivyo alisema Jerry Muro kuhusu sakata la kufukuzwa Yanga.

No comments:

Post a Comment