Thursday, July 16, 2015

Manchester United kumuuza Victor Valdes baada ya kukataa kucheza nafasi ya golikipa wa akiba (Reserves)


Golikipa Victor Valdes atauzwa na manchester United baada ya Manager Louis Van Gaal kuthibisha kuwa golikipa Victor Valdes alikataa kucheza nafasi ya golikipa wa akiba katika msimu wa mwaka jana ambao ulimazika kwa Valdes kuwa golikipa wa akiba (Reserve)


Golikkipa huyo wa kimataifa wa hispania alihamia Manchester United kwa uhamisho wa bure akitokea Barcelona katika msimu wa 2013/ 2014 wakati mkataba wake ulipo malizika. kuwa katika kikosi cha Manchester United ilimsaidia kuweza kuwa katika kiwango kizuri lakini kwa kufuatia jeraha la goti ambalo lilimuweka nje katika fainali za kombe la dunia mwaka 2014, Victor Valdes alipata dili la kusajiliwa na Manchester United  na kuja kuwa golikipa wa ziada mbadala ya golikipa David De Gea.

Kocha Louis Van Gaal amethibitisha kutaka kumuuza Valdes baada ya kuonesha kuwa golikipa huyo amekuwa haamini falsafa za mdachi Louis Van Gaal, lakini pia kukosekana katika kikosi kitakacho kwenda katika ziara nchini marekani Van Gaal amesema kwamba hadhani kama Victor Valdes atakuwa na nafasi ya kuendelea kubaki Old Trafford.

No comments:

Post a Comment