Thursday, July 2, 2015
Antonio Rudiger anatakiwa na Chelsea pamoja Wolfsburg
Klabu ya Chelsea na klabu ya Wolfsburg ya Ujerumani vinataka kumsajili beki wa kati wa klabu ya Stuttgart ya nchini Ujerumani, Gazeti la "Bild" liliripoti kuwa Beki huoy wa Stuttgart, Antonio Rudiger ameshakubaliana na klabu ya Wolfsburg katika masharti ya kimkataba na klabu hiyo lakini bado vilabu hivyo viwili vinafanya makubaliano na beki huyo wa Stuttgart huku klabu ya Stuttgart ikitaka ada ya paundi milioni 18 ilikuweza kumuachia Antonio Rudiger.
Wakala wa Antonio Rudiger aliliambia gazeti la "Kicker sport magazine" kwamba "Najua kuhusiana na vilabu vya Chelsea na Wolfsburg kutaka kumchukua Antonio Rudiger" alisema wakala wa Antonio Rudiger.
Antonio Rudiger mwenye umri wa miaka 22 amecheza mechi 19 akiwa na klabu ya Stuttgart licha ya jeraha la muda mrefu lililomfanya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment