ligi kuu ya Tanzania ilimalizika mapema katika mwezi wa tano ambapo mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania ni Yanga Sports club. Yanga waliwanyang'anya kombe la ubingwa wa ligi kuu wana wa lambalamba Azam Fc ambao wao walikuwa mabingwa watetezi wa ligi hiyo, baada ya ligi kuisha baadhi timu ziliweza kushuka daraja na zingine kuweza kuendelea kushiriki ligi kuu kwa msimu ujao, timu ambazo zimeweza kupanda na kuweza kupata nafasi ya kushiriki ligi kuu kwa msimu wa 2015/2016 ni African sports, majimaji, Mwadu Fc pamoja na Toto Africans timu hizo zitaungana na timu ambazo zimebaki katika ligi kuu. timu hizo nne zilizo panda daraja zitafanya sasa ligi kuu ya Tanzania bala kuwa na tim 16 zinazoshiriki ligi hiyo.
Hizi ndizo timu 16 ambazo zitashiriki ligi kuu Tanzania bala kwa msimu wa 2015/2016
No comments:
Post a Comment