Thursday, July 16, 2015

Klabu ya Leicester City yaweka imani kwa Esteban Cambiasso kuongeza mkataba mpya


Klabu ya Leicester City imekuwa na tumaini la kumshauri mchezaji Esteban Cambiasso kuongeza mkataba mpya kufuatia uteuzi wa Boss wa zamani wa klabu ya Intermilan, Claudio Ranieri ambaye kwa sasa ameinunua klabu ya Leicester City, Claudio Raniera anamtaka Combiasso kuongeza mkataba wa miaka mitatu katika ya klabu ya Leicester City.


Boss Claudio Raniera anaamini kwamba yeye tayari ameshapewa nafasi ya mkurugenzi wa michezo katika klabu ya Lecister City. huku wa Leicester city, jon Rudkin akiwa amepewa orodha ya majina ya usajili wa klabu hiyo kwaajili ya msimu ujao wa ligi kuu nchini Uingereza.

Mpaka sasa klabu ya Leicester City imeshafanya usajili wa beki wa kulia Christian Fuchs akitokea katika klabu ya Schalke 04 ya Ujerumani pamoja na straika kutoka nchini Japan Shinji Okazaki kwa ada ya uhamisho wa paundi milioni 7.5 akitokea katika klabu ya Mainz 05 ya Ujerumani. Leicester City pia wamevutiwa kutaka kumsajili kwa mkopo Robert Huth  kutoka Stoke City lakini pia wakitaka kumchukua Jeffrey Schlupp paomja na Mancini Wasilewski.

klabu ya Leicester City imeweka wazi kuwa mshambuliaji wao hatari Esteban Combiasso ataongezea mkataba mpya wa kuendelea kubaki katika klabu ya Leicester City mpaka pale mkataba wake utakapomalizika.


No comments:

Post a Comment