Tuesday, July 7, 2015

Kevin Prince-Boateng anaweza kusajiliwa na Galatasaray au AC Milan


Wakala wa mchezaji wa kimataifa wa Ghana, Kevin Prince-Boateng  amesema kwamba mshambuliaji wa Schalke 04 ya Ujerumani, Kevin Prince-Boateng anaweza kujiunga na klabu ya Galatasaray au anaweza kurudi katika klabu yake ya zamani ya AC Milan.


Boateng ambaye kwa sasa anatafuta klabu yakuweza kuichezea baada ya kusimamishwa katika klabu ya Schalke 04 kwa kitendo cha utovu wa ni dhamu, huku wakala Boateng anayeitwa Eduardo Crnjar alisema kwamba klabu ya Galatasaray inamuhitaji Boateng wakati Boateng mwenyewe akisema kwamba anataka kurejea katika klabu ya AC Milan.

Lakini pia vilevile wakala Eduardo Crnjar alisema "Sijui kama Boateng atasajiliwa na Galatasaray au  kucheza katika klabu yake ya zamani ambayo ni AC Milan, sijui kwa kweli labda chochote kinaweza kutokea" alisema Crnjar ambaye ni wakala wa Kevin Prince Boateng.

No comments:

Post a Comment