Thursday, July 2, 2015
Rickie Lambert yupo tayari kuondoka Liverpool
Strika wa Liverpool, Rickie Lambert amethibitisha kuwa anatarajia kuondoka Anfield msimu huu, Lambert ambaye alikuwa katika kupambana kuhakikisha anarudisha kiwango chake baada ya usajili wake wa kushtukiza akiwa anatokea Southampton msimu uliopita wakati huo Aston Villa alikiwa ikisikika kumwania straika huyo wa Uingereza.
Pamoja na kujitahidi sana kufanya vizuri na klabu yake ya nyumban, Lambert alitegemea kuendelea kubaki Anfield hadi msimu ujao na huku ikonekan straika huyo mwenye umri wa miaka 33 anajiandaa kuondoka Liverpool na kutafuta timu nyingine yakuitumikia kwa msimu mpya wa English Premier League.
Kusajiliwa kwa wachezaji nyota Danny Ings kutoka Burnley na Roberto Firmino akitokea 1898 Hoffeneim ya Ujerumani wachezaji nyota hao watakao kuja kwaajili ya msimu mpya wa English Premier league utakaoanza kutimua vumbi mwezi wanane, Ambapo usajili wa nyota hao katika klabu ya Liverpool ndiyo unaomfanya Rickie Lambert kutegemea kuondoka Anfield, huku maisha ya nyota Mario Baloteri na Fabio Borini na wao pia wapo hatiani kuonoka Liverpool.
Baadaa ya Rickie Lambert kusema kuwa hataraji kuendelea kubaki Anfield klabu ya West Bromwich imejitokeza kutaka kumsajili Rickie Lambert huku Kocha wa Crystal Palace, Allen Pardew ambaye alimsajili Lambert mwaka 2009 katika klabu ya Southampton naye pia Allen Pardew amekuwa akisikika kutaka kumsajili Rickie Lambert katika klabu yake ya Crystal Palce.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment