Saturday, July 4, 2015

Yanga SC yakubali yaishe baada Kiiza kusajiliwa na Simba SC


Kitendo cha strika Hamis Kiiza "Diego" kusaini mkataba wa kucheza Simba SC kimeweza kuwatetemesha wana wajangwani Yanga SC baada ya nahodha wa Yanga Nadir Haroub "Cannavaro" kukili kuwa Hamis Kiiza ni moja kati ya washambuliaji hatari sana.


Cannavaro ambaye aliweza kucheza na Kiiza kwa misimu kadhaa wakati kiiza akiwa anacheza Yanga, Cannavaro aliweza kutaja moja ya sifa ya Hamis Kiiza anapokuwa katika eneo la lango huwa Kiiza lazima atakuliza awezavyo. Nadir Haroub "Cannavaro" alisema "Kiiza yupo makini kuangalia beki anafanya nini na mara nyingi uchezaji wa hivyo ni hatari sana na lazima kama beki uwe na akili ya ziada kuhakikisha unambana ipasavyo, hata Simba wanakumbuka alivyokuwa akiwaliza  ndiyo maana wamemdaka ili aweze kuwabeba" alisme beki Cannavaro.

Nahodha Cannavaro alisema kuwa haitakuwa rahisi kwa Kiiza kupenya ovyo ngome ya Yanga kutokana na maandalizi wanayoyafanya na jinsi wanavyo mfahamu Kiiza "Diego" hata hivyo straika huyo atawapa wakati mgumu wakuweza kumkabili.

Cannavaro aliendelea kwa kusema kuwa "Simba SC imepata kifaa cha ukweli, Sio kuachwa na Yanga ndiyo kiwango chake kimeshuka bali ni mahitaji ya kocha anapotaka wachezaji anaowataka kwa wakati husika" alisema

Hata hivyo kwa upande wa mashabiki wa Yanga SC juzi Jumatano walimponda straika Kiiza kuwa aliweza kushuka kiwango kwa miaka miwili na ndiyo maana hakuwa katika nafasi ya kocha kuweza kumchezesha Kiiza katika kikosi cha kwanza. Hamis Kiiza ambaye aliichezea Yanga SC kwa misimu miwili na kusajili na Simba SC hivi karibuni kwa mkataba wa miaka miwili wa kuichezea Simba.

No comments:

Post a Comment