Sunday, June 14, 2015

Inter-milan yakomaa na Yaya Toure.

Manager wa club ya Intermilan, Roberto Mancini, ameendelea kulazimisha kumsajili midfielder wa club ya Manchester City, Yaya Toure licha ya Manchester City kukataa kumuuza Yaya Toure kwenda club yoyote balani ulaya lakini Roberto Mancini analazimisha kutaka kumsajili mchezaji huyo wa Manchester City.

Roberto Mancini ambaye alikuwa manager wa club ya Manchester City kwa misimu miwili akitokea katika club ya Intermilan ambayo ndiyo kocha mkuu wa club hiyo kwa sasa. wakati yupo Manchester City Mancini aliweza kiupa club hiyo ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza alimaarufu kama English Premier League (EPL). baada ya kuweza kuipa ubingwa club hiyo alitimuliwa na club hiyo na kwenda kuinoa club ya Galatsary  ya nchini Uturuki na baada ya hapo alirudi katika club yake ya zamani ambayo ni club ya Intermilan.

Mancini ameendelea kuweka mkazo wakutaka kusajili Yaya Toure anaecheza katika club ya Manchester City licha ya kwamba club ya Manchester City imesema kwamba haipo tayari kumuachia mchezaji huyo ili ajiunge na club nyingine, lakini bado manager Roberto Mancini anakomaa na kutaka kumsajili Yaya Toure.

No comments:

Post a Comment