Timu ta Taifa ya Tanzania (Taifa stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro premium lager imepoteza mchezo wake wa kwanza wa kuwania kufuzu kwa fainali za AFCON 2017 ambazo zitafanyika nchini Gabon.
Taifa stars ilianza kwa kucheza vizuri katika kipindi cha kwanza has katika eneo la ulinzi na kuweza kumaliza kipindi cha kwanza bila kufungana huku mabeki wa Taifa stars waliweza kufanya kazi ya ziada kuzuia mashambulizi ya Misri.
Kipindi cha kilipoanza Misri ilifanya mabadiliko ambayo ndio yalikuwa chachu ya kupatikana kwa mabao matatu ndani ya kipindi cha pili. Mabao ya Misri yalifungwa ndani ya dakika 10 ambapo mabao ya Misri yalifungwa na Ramy Rabia ambaye alifunga bao la kwanza katika dakika ya 60, Basem Morsy dakika ya 64, na Mohamed Salah ambaye alifunga goli la tatu katika dakika ya 69.
Taifa stars ilifanya mabadiliko na kumuingiza Frank Domayo, Simon Msuva pamoja na Salim Mbonde na Stars ilifanya mashambulizi kadhaa katika lango la Misri lakini mashambulizi hayakuzaa matunda.
Matokeo mengine ya kuwania kufuzu AFCON 2017 ni kama yafuatavyo:
Togo - Liberia (2-1), DRC Congo - Madagascar (2-1), Equateriol Gueinea - Benin (1-1), Congo - Kenya (1-1), Mozambique - Rwanda (0-1), Ghana - Mauritus (7-1), Sudan - Sierra Leone (1-0), Ethiopia - Lesotho (2-1), Niger - Namibia (1-0), na Cameroon - Mauritania ( 1-0).
No comments:
Post a Comment