Thursday, July 2, 2015
Sergio Ramos aiambia Real Madrid kuwa anataka kwenda Manchester United
Beki wa kimataifa wa Hispania, Sergio Ramos ameiambia Real Madrid kuwa anataka kuondoka na kwenda zake kujiunga na klabu ya Manchester United kwa mujibu wa gazeti la The Gurdian la nchini Uingereza. Ramos mwenye umri wa miaka 29 amekuwa aikitaarifiwa na magazeti ya nchini Hispania kwa kuasjiliwa na Manchester United kwa ada ya paundi milioni 40, huku kituo cha habari za michezo nchini Uingereza (Sky sport news) kikiripoti kuwa kumekuwa na offer zingine zinazotakiwa kutolewa na klabu ya Manchester City kawa kutaka kumsajili Beki huyo wa Real Madrid.
Mbali na ripoti hizo mbalimbali za usajili wa Ramos, Kituo cha ESPN cha Uingereza kiliripoti kuwa Manchester United haitaweza kuongeza dau jingine zaindi paundi milioni 40 wakati Real Madrid wakitangaza dau lao la kutaka paundi milion 65 kwa kumuachia Sergio Ramos dau ambalo litavunja rekodi ya usajili nchini Uingereza baada ya lile la paundi la milioni 59.7 wakati Manchester United ikimsajili Angel Di Maria akitokea Real Madrid.
Lakini licha ya kwamba Real Madrid ilikata offer ya kwanza iliotolewa na klabu ya Manchester United na wakati bado Kocha wa Manchester United Luis Va Gaal anakitita cha hela kiasi cha paundi milioni 150 kwaajili ya usajili msimu lakini klabu hiyo ya Ungereza haitaki kuingia katika matatizo ya kiuchumi.
Usajili wa Sergio Ramos hata kwa dau la paundi milioni 40 unawezekana lakini kwa kutegemea na kiwango cha ubadilishaji wa fedha duniani. Sergio Ramos ni moja kati ya wachezaji wenye mafanikio makubwa katika klabu aya Real Madrid ambapo ameweza kuchukua mataji mbalimbali ikiwamo taji la ligi ya mabingwa nchini hispania (La Liga) ubingwa wa mabingwa balani ulaya UEFA champions League na hata baadhi ya mataji ya kimataifa kama ubingwa wa kombe la dunia walilochukua mwaka 2010 pamoja na taji la ubingwa wa fainali za EUROPEAN champions.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment