Thursday, July 2, 2015

Klabu ya Juventus yakataa offer ya puandi milioni 80 iliyotolewa na FC Barcelona


Klabu ya Juventus ya nchini Italy imekataa offer ya paundi milioni 80 iliyotolewa na Barcelona kwaajili ya uhamisho wa midfielder Paul Pogba. Mkurugenzi mtendaji wa klabu ya Juventus, Giuseppe Moratta amethibisha kwamba nyota huyo chipukizi kutoka Ufaransa hayupo katika mauuzo na havyo Juventus haina mpango wakumuuza Paul Pogba.


Pogba mwenye umri wa miaka 22 ni moja kati ya wachezaji nyota wanaowaniwa kusajiliwa na vilabu kubwa balani ulaya hari inafanya kuwa ni moja ya chaguo na baadaye kwa klabu ya Barcelona licha ya kwamba Barcelona wamefungiwa kusajili wachezaji hadi mweni January 2016.

Giuseppe Moratta aliliambia gazeti moja la nchini Italy (Gazzeta Della sport) Moratta alisema "Tulipokea offer ya paundi milioni 80 kutoka Barcelona lakini hatujaridhia kama tutamuuza Paul Pogba" alisema Moratta ambaye ni Mkurugenzi mtendaji wa klabu ya Juventus.

Mgombea urais wa klabu ya Barcelona Joan Laporta alisema kwamba anategemea kumsajili midfielder Paul Pogba indapo tu atachaguliwa tena kwa mara ya pili mwenzi ujao katika uchaguzi wakumpata rais wa klabu ya Barcelona. Barcelona haitakuwa na rais au bodi mpaka baada ya uchaguzi kumalizika tarehe 18 July.

Kiungo Paul Pogba amekuwa akihusishwa kusajiliwa na vilabu vikubwa balani ulaya kama Manchester City, Manchester United, Real Madrid na Paris Saint German licha ya offer ya paundi milioni 100 kukataliwa.

Chombo cha habari cha klabu ya Barcelona (Catalan Media) kilikutana na maafisa wa klabu ya Juventus hapo jana Jumatano na walikubaliana kuhusu usajili wa kiungo Paul Pogba lakini offer yao ya kutaka kumchukua Paul Pogba imekataliwa.


No comments:

Post a Comment