Wednesday, July 1, 2015

Azam FC kujiandaa na michuano ya Kagame Cup 2015


Klabu ya Azam Fc imeweka nia yakutaka kufanya vizuri katika michuano ya CECAFA Kagame Cup 2015 kwa upande wa vilabu ambayo yanakaribia kutimua vumbi hivi karibuni. Ikiwa ni punde tu ratiba ya Kagame Cup 2015 ikiwa imetolewa hi leo ambapo kuna idadi ya makundi matatu na kila kundi lina idadi ya timu tano huku Tanzania ikwakirishwa na Yanga SC pamoja na Azam Fc.


Klabu ya Azam yenyewe imeweka kambi yake katika uwanja wake nyumbani uliopo chamanzi nje kidogo ya mji wa Dar es Salaam, Azam Fc imekuwa ikijiandaa na michuano hiyo ya Kagame Cup lakini pia wamekuwa wakijiandaa na ligi kuu Vodacom ambayo itaanza kutiomua vumbi mwezi wa nane (8) huku ikijiandaa pia na michuano ya kombe shirikishi la mataifa ya Afrika ambapo Azam Fc itashiriki michuano hiyo.

Mbali na harakati hizo za kujiandaa na michuano mbalimbali klabu ya Azam Fc imeweka nia yakutaka kufanya vizuri na hata kuweza kuchukua kombe la CECAFA Kagame Cup kwa mwaka wa 2015 klabu hiyo ipo katika maandalizi hayo ya kuhakikisha wanafanya vizuri katika michuano hiyo kwani kwa miaka mingi wamekuwa wakifanya vibaya wakiwa wakiishia hatua ya makundi lakini pia hata kutolewa katika hatua ya robo fainali sasa safari hii Azam Fc ikiwa chini ya Muingereza Stewart Hall ambaye ameleje tena kuifundisha klabu hiyo baada ya kutimuliwa mwaka 2014 na nafasi yake ilichukuliwa na Joseph Omog lakini pia na yeye ametimuliwa na hatimaye Muingereza huyo kuweza kurejea tena katika klabu ya Azam Fc na kuifundisha tena kwa mara ya pili.

No comments:

Post a Comment