Wednesday, July 1, 2015
Kimondo FC yaikalia kooni Yanga SC.
Baada ya kufanya vizuri katika mechi ya kirafiki baina ya Yanga SC dhidi ya SC Villa mchezo uliochezwa siku ya jumamosi iliyopita ambapo Yanga SC ilitoka sare dhidi ya SC Villa ya nchini Uganda, Baada ya mchezo huo kumalizika siku chache zilizopita hii leo amejitoza mlezi \wa klabu ya Kimondo FC Bwana Eric Ambakysie aliibuka na kudai kuwa mchezaji wa Yanga SC aliyesajiliwa hivi karibuni yeye bado ni mali ya klabu ya Kimondo FC na mchezaji huyo ana mkataba wa miaka minne (4) na klabu ya Kimondo FC.
Akizungumza na wahandishi wa habari hii leo mkurugenzi wa kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu ya Yanga SC, Jerry Muro alisema kuwa mchezaji aliyesajiliwa na Yanga SC hana mkataba wowote na klabu ya Kimondo Fc na hivyo wasilete zakuleta kutaka kumchukua mchezaji huyo baada ya kuonesha kiwango kizuri katika mechi ya kirafiki dhidi ya SC Villa." alisema Jerry Muro
Kimondo Fc klabu ambayo itashiriki ligi daraja la kwanza kwa mwaka wa 2015/2016 ambapo ipo katika kundi B katika makundi ya ligi kuu daraja la kwanza. Kimondo Fc ambayo ilikuwa ikimmiliki mchezaji huyo ambaye amesajiliwa na Yanga SC klabu hiyo imeweza kuja juu kwa kudai kuwa mchezaji aliyesajiwa Yanga SC bado ni mchezaji halali wa Kimondo Fc na bado mchezaji huyo ana makataba na klabu ya Kimondo Fc.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment