Monday, June 22, 2015
Yanga yasema jambo kuhusu Mkwasa kuifundisha Taifa Stars.
Kutokana na jina la kocha msaidizi wa Yanga SC Charles Boniface Mkwasa kutajwa kuwa kocha wa Taifa stars kwa kipindi cha mpito, Uongozi wa Yanga SC umevunja ukimya wa uteuzi wa kocha mzalendo kuja kuinoa Taifa Stars baada ya Mart Nooij kutimuliwa kazi pamoja na benchi zima la ufundi. Yanga imelivunjia kauli uteuzi wa Mkwasa kuja kuifundisha Taifa Stars, katibu mkuu wa Yanga SC Dokta Jonas Tiboroha amesema Yanga bado inmuhitaji Mkwasa kwa aajili ya maendeleo yake ya soka akiwa na Yanga SC na kama watamruhusu Mkwasa kuifundisha Taifa Stars kwa muda na siyo muda mrefu.
Akizungumza na waandishi wa habari Katibu mkuu wa Yanga dokta Jonas Tiboroha alisema ya fuatayo kuhusu uteuzi wa Mkwasa kuwa kocha wa mpito katika timu ya taifa, alisema.
"Mimi kwa kujibu harakaharaka tu kwa kuwa sijawasiliana na viongozi wenzangu kuhusu hilo swala wala mwalimu hajaniambia kuhusu hilo jambo ila nataka watu wajue kwamba kocha Boniface Mkwasa ana mkataba na Yanga na kwa maana hiyo lazima uwepo muafaka baina ya Yanga na TFF utakao mruhusu Boniface Mkwasa kuwa kocha wa Timu ya taifa kitu ambacho nakiona ni kigumu labda kama itakuwa kwenye part time engagement."
Dokta Jonas Tiboroha aliendelea kwa kusema, "Lakini on full time basis siioni hiyo kutokea sasahivi kwasababu bado Mkwasa ana mkataba na Yanga SC na mkataba wake hauishi leo wala kesho, Unajua kuna mambo mengine tunataka kuyabadilisha kwa maslahi ya kitaifa ndio maana tumesema Yanga tunaweza kumruhusu Mkwasa kuwa kocha wa Taifa stars kwa part time basis na siyo kwa full time basis" alisema Jonas Tiboroha.
Jina la Charles Boniface Mkwasa ndio jina pekee lilotajwa na TFF kuwa ndio kocha wa muda atakayerithi mikoba ya Mart Nooij ambaye ameshakwishatimuliwa kazi na TFF kutokana na matokeo mabaya waliopata Taifa stars wakati wakicheza mchezo wao wa kwanza wa kufuzu michuano ya CHAN ambapo Tanzania ilicheza dhidi ya Uganda na Tanzania kupewa kichapo cha mabao 3-0 katika mchezo huo ambao ulichezwa visiwani Zanzibar.
Baada ya TFF kutrangaza kumfukuza kazi Mart Nooij pamoja nabenchi zima la ufundi TFF kupitia kamati ya Utendaji ilitangaza jina la Boniface Mkwasa kuwa ndio kocha wa mpito wa timu ya taifa ambapo taarifa hiyo ilitolewa hapo jana June 21.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment