Monday, June 22, 2015

Peter Cech ataibadirisha Arsenal kuweza kuchukua ubingwa wa EPL.


Baada ya miaka mingi kupita club ya Arsenal ikiwa haijachukua taji la ubingwa wa ligi kuu nchini Uingereza (EPL) hatimaye kocha Arsen Wenger amefikia hatua ya kumsajili golikipa wa Chelsea, Peter Cech. Golikipa Peter Cech amekuwa akilripotiwa kuwa ameshawasiri katika uwanja wa Emirate wa Arsenal akiwa tayari kujiandaa kwa kujiunga na club hiyo ya kaskazini mwa London.

Arsenal imekuwa na tatizo kwa upande wa golikipa kwa miaka kadhaa baada ya goilkipa Jens Lehman kumaliza soka akiwa na club ya Arsenal, Golikipa Lehman alikuwa na mchango mkubwa sana katika mafanikio ya Arsenal hasa yale yakuchukua ubingwa wa English Premier League mwaka 2004 bila hata kupoteza mchezo hata mmoja (Unbeaten) lakini baada ya muda tu kiwango cha golikipa Lehman kilianza kushuka na hapo ndipo kocha Arsen Wenger aliona umuhimu wa kumsajili golikipa Manuel Almunia ambaye alichukua nafasi ya Jens Lehman.


Manuel Almunia aliichezea club ya Arsenal kwa misimu mitatu baada tu ya kusajili na Arsenal, Almunia aliweza kufanya vizuri sana mwanzoni mwa msimu wake wa kwanza akiwa Arsenal lakini baadaye alianza kufanya vibaya hari iliyompelea Wenger kutafuka golikipa mwengine wakuja kuchukua nafasi ya Manuel Almunia na ndipo Wenger akamsajili golikipa Wojciech Szczesny ambaye yupo mpaka sasa katika club ya Arsenal.

Usajili wa Peter Cech wa Chelsea umeweza kupata headlines nyingi kwenye magazeti mengi balani ulaya huku ikiwa wazi kwamba Peter Cech ameridhia kwenda katika club ya Arsenal. Usajili wa Peter Cech utakuwa ni wa mchango mkubwa sana katika club ya Arsenal kwa mafanikio ya kuchukua ubingwa wa ligi lakini pia hata kuchukua kombe la mabingwa balani ulaya, Mpaka sasa Peter Cech ameweza kushinda mataji 13 akiwa na Chelsea.


Takwimu za msimu wa 2014/2015 ambao umemalizika huku ikionyesha golikipa Peter Cech akiwa na wastani mzuri kwa kiwango alichonacho wakati akiwa Chelsea ambapo akiwa Chelsea ameweza kucheza mechi 7 tu na akiwa na asilimia ya uokoaji ni 88.9% ambayo amewazidi magolikipa wa Arsenal.

No comments:

Post a Comment