Monday, June 22, 2015

Mario Mandzukic amesajiliwa na Juventus


Club ya Juventus ya nchini Italy imekamilisha dili la kumsajili mchezaji wa Atletico Madrid, Mario Manduzukic mwenye umri wa miaka 28. Mandzukic aliyetokea katika club ya Bayern Munich wakati akisajiliwa na Atletico Madrid na kuichezea Atletico Madrid kwa msimu mmoja na hatimaye sasa amesajiliwa na club ya Juventus.


Juventus imemsajili Mario Mandzukic kwa dau la paundi milioni 15 akitokea Atletico Madrid, Mario Mandzukic ambaye aliweza kufanya vizuri sana akiwa na Atletico Madrid kiasi cha kwamba ilipelekea vilabu mbalimbali vikitaka kumsajili ikiwamo Manchester United ambayo ilikuwa ikmuhitaji Mario Mandzukic.

Juventus iliweka dau ambalo liliweza kuishawishi club ya Atletico Madrid kumuachia Mario Mandzukic, usajili wa Mandzukic kwenda Juventus unaziba nafasi ya Carlos Tevez ambaye inasemekana ataondoka Juventus na kwenda kijiunga na club nyingine ambapo club ambazo zimekuwa zikitajwa kutaka kumsajili Tevez ni pamoja na club ya Paris saint German (PSG).

Mario Mandzukic ndiyo saini ya kwanza ya Juventus kumsajili mchezaji huyo anayetokea Atletico Madrid, Juventus ambayo kwa sasa inahusishwa na kutaka kuwasijili wachezaji wengine katika club hiyo ili kuweza kushindana na vilabu vingine katika michuano ya UEFA champions league  ambayo huwa inakutanisha vilabu vya mabingwa balani ulaya.

Usajili wa Mario Mandzukic umekamilika kwa ada ya paundi milioni 15 akiwa antokea katika club ya Atletico Madrid ya nchini Hispania.

No comments:

Post a Comment