Tuesday, June 9, 2015

Yanga Sports Club yajiandaa na michuano ya CECAFA.

Wakati ligi kuu bala imemalizika na bingwa wa ligi kuu akiwa ni Yanga Sports Club ambao wametwaa ubingwa huo kwa mwaka huu na kuwapokonya taji wana walambalamba Azam FC ambao ndio walikuwa mabingwa watetezi wa ubingwa huo wa ligi kuu bala. lakini baada ligi kumalizika sas ni zamu ya michuano ya Afrika mashariki na kati ambayo huzikutanisha timu za kutoka jumuiya ya Afrika mashariki pamoja na zile za Afrika ya kati.

Timu ambazo zinazotokea kwa upande wa Afrika mashiriki ni zile za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi wakati zile za afrika ya kati ni timu za nchi ya Sudan, Somalia, Ethiopia na zinginezo. Michuo ya CECAFA  inakaribia kuanza na hivyo timu ya Yanga Sports club ipo katika maandalizi ya kujiandaa na michuano hiyo ya Afrika mashariki na kati.

No comments:

Post a Comment