Tuesday, June 9, 2015

Juventus yamsajili Sami Khadira kutoka Real Madrid.

Kiungo wa club ya Real Madrid, Sami Khadira mwenye umri wa miaka 28 amesajiliwa na club ya Juventus ya nchini Italy. Juventus wamethibitisha wazi kuwa wamemsajili kiungo wa Real Madrid, ikumbukwe  kuwa Sami Khadira ameichezea Real Madrid kwa karibu misimu mnne akiwa katika club hiyo na vilevile alichangia kwa namna moja au myingine kuiwezesha Real Madrid kuchukua kombe la Mfalme (Cop de Ley) pamoja na ubingwa wa ligi ya mabingwa balania ulaya kwa mwaka wa 2014/2015.

No comments:

Post a Comment