Saturday, June 27, 2015
Yanga SC kukipiga na SC Villa ya Uganda hii leo.
Mabingwa wa ligi kuu kwa msimu wa 2015/2016 ligi kuu ya Vodacom ambayo ilimalizika mwishoni mwa mwezi wa tano, Yanga SC ambayo iliweza kuchukua ubingwa wa ligi kwa kuweza kuipiku klabu ya Azam FC ambao ndiyo walikuwa mabingwa watetezi kwa msimu uliomaliza Lakini kwa msimu uliomalizika Yanga SC iliweza kuibuka kuwa mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom.
Baada ya ligi kuu kumalizika wachezaji wa klabu ya Yanga SC walikwenda mapumzikoni kwa kuweza kupumzika kwa kipindi ambacho ligi ilikuwa imemalizika lakini pia kuna wale wachezaji ambao waliweza kuitwa kwenye vikosi vya timu zao za taifa ambapo walijumuika na wenzao katika vikosi vyao vya timu ya taifa. kwa upande wa klabu ya Yanga SC wachezaji ambao waliweza kuitwa katika kikosi cha timu ya taifa ni Narid Haroub "Cannavaro", Kevin Yondani, Juma Abdul pamoja na Simon Msuva ambao waliweza kujiunga na wachezaji wengine walioitwa katika kikosi cha timu ya taifa punde tuu baada ya ligi kumalizika.
Wakati baadhi ya wachezaji wa Yanga SC wakiwa wanatumikia timu zao za taifa klabu ya Yanga SC ilikuwa ikiendelea na harakati za kusajili wachezaji wengine ambao watakuja kujumuika na wachezaji wengine waliobaki katika klabu ya Yanga.
Yanga SC baada ya kufanya usajili wa wachezaji katika klabu hiyo ambapo wachezaji waliosajiwa na klabu hiyo ni pamoja na wale wa ndani na nje ya nchi, Yanga SC itashuka dimbani hii leo kupambana katika mchezo wa kirafika dhidi ya klabu ya SC villa ya nchini Uganda mchezo ambao utachezwa katika uwanja wa Taifa.
Mchezo huo ambao Yanga SC itacheza dhidi ya SC villa itakuwa ni sehemu ya klabu ya Yanga kuweza kuwatambulisha wachezaji waliosajiwa katika klabu hiyo ambapo wachezaji hao watatambulishwa mbele ya mashabiki wa klabu ya Yanga SC, Mbali na utambulisho huo wa wachezaji wa klabu ya Yanga pia kutakuwa na burudani kutoka Ya moto Band ambao watatoa burudani kwa mashabiki watakaoweza kufika uwanjani hapo kuweza kushuhudia mchezo huo.
Mapato yatakayopatikana katika katika mchezo huo yatakwenda kusaidia watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) ambapo klabu ya Yanga SC haitachukua shilingi hata moja itakayotokana na mapato ya mchezo huo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment