Wednesday, June 24, 2015

Mkwasa aitisha kikosi cha Taifa stars.


Kocha wa timu ya taifa "Taifa stars" Charles Boniface Mkwasa leo ametangaza kikosi cha Taifa stars ambacho kitaanza kuweka kambi kwaajili ya kujianda na mechi ya marudiano dhidi ya Uganda katika michuano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza soka ndani ya nchi (CHAN) ambapo katika mechi ya awali Taifa stars iliweza kukubali kipigo cha mabao 3-0 dhidi ya Uganda (The Cranes) mchezo ambao ulichezwa visiwani Zanzibar.


Licha ya kuchagua kikosi kipya cha wachezaji 26, Kocha Mkwasa alisema vipaumbele vyake ambavyo alivizingatia wakati akiteua majina ya wachezaji watakao itumukia timu ya taifa na kuweza kufanya vizuri katika mechi za marudiano, Mkwasa alisema kwamba kitu pekee alichokizingatia katika kuchagua majina hayo 26 ya wachezaji ni kitu cha nidhamu ambacho ndiyo msingi mkuu wa timu kuweza kufanya vizuri. Kocha Mkwasa kabla ya kutaja wachezaji 26 aliowachagua kwanza alianza na benchi kuu la ufundi ambalo alilitaja kama ifuatavyo, Kocha msaidizi ni Hemed Morocco, Kocha wa makipa Peter Manyika, Mtunza vifaa (Hussein Sued), Msahuri wa timu (Abdallah Kibaden), Mratibu wa timu (Alhaji Ahmed Idd Mgoyi) na Meneja wa timu (Juma Mgunda) hilo ndilo benchi la ufundi lililotajwa na kocha Boniface Mkwasa ambalo atakuwa akishirikiana nalo kuhakikisha wanapata matokeo mazuri katika michuano ambayo Tanzania itakuwaikishiriki.

Mbali ya kutaja benchi la ufundi Kocha Mkwasa aliweza kutoa shukrani zake kwa shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) kwa kuweza kumteua kuwa kocha wa Timu ya Taifa kwa kipindi cha mda mfupi mpaka pale TFF itakapo pata kocha wakuja kuifundisha Taifa stars baada ya kocha Mart Nooij kutimuliwa kutokana na mfurulizo wa matokeo mabaya ambayo Tanzania imekuwa ikiyapata kwa mechi ambazo Tanzania imecheza, Mkwasa pia hakusita kuweza kutoa shukrani zake kwa klabu ya Yanga SC kwa kuweza kumruhusu kuifundisha Taifa stars kwa kipindi hiki ambacho jahazi la Tanzania linakaribia kuzama, Boniface Mkwas alimalizia kwa kusema kwamba kufundisha timu ya taifa siyo kazi rahisi bali lolote linaweza kutokea ila ninaomba ushirikiano wenu katika kuifanikisha taifa stars inafanya vizuri.

Baada ya kusema machache hayo kutoka kwa kocha Boniface Mkwasa sas ilifika muda wakutaja kikosi kipya cha Taifa stars ambacho kitaanza kuweka kambi kwaajili yakujiandaa na mechi za marudiano, Kikosi cha Taifa stars ni kama kifuatavyo:

Magolikipa
(1)Mudathir Khamis  (KMKM)
(2)Mwadini Ali    (Azam FC)
(3)Mustapha ally "Barthez"  (Yanga SC)

Mabeki
(4)Shomari kapombe (Azam FC)
(5)Michael Aidan (Ruvu shooting)
(6)Mohammed Hussein "Tshabalala"  (Simba SC)
(7)Mwinyi Ally Mngwila (KMKM)
(8)Nadir Haroub "Cannavaro"   (Yanga SC)
(9)Kevin Yondani  (Yanga SC)
(10)Agrey Morris  (Azam FC)

Viungo
(11)Jothan Mkude  (Simba SC)
(12)Abdi Banda  (Simba SC)
(13)Salum Telela (Yanga SC)
(14)Frank Domayo   (Azam FC)
(15)Simon Msuva    (Yanga SC)
(16)Said Ndemla     (Simba SC)
(17)John Bocco     (Azam FC)
(18)Ramadhan Singano "Messi"   (Simba SC)
(19)Deus Kaseke (Mbeya City)

Washambuliaji
(20)Atupele Green  (Kagera Sugar)
(21)Rashid Mandawa (Kagera Sugar)
(22)Ame Ally  (Mtibwa Sugar)

Waliowekwa pembeni (Reserve) ni pamoja na Mudathir Yahya (Azam FC), Juma Abdul (Yanga SC), na Samuel Kamuntu (JKT Ruvu).

Na hicho ndicho kikosi kipya kilichotajwa hii leo na kocha Boniface Mkwasa akiwa pamoja na benchi lake la usaidizi. Kesho benchi la ufundi litakutana na wachezaji waliotajwa ili kuweza kuwajengea uzalendo, wachezaji waliotajwa watakutana katika hoteli ya Tansoma ya jijini Dar es Salaam na kocha Mkwasa akasema timu ya taifa itaanza kuweka kambi yake nje ya mji wa Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment