Monday, June 29, 2015

Beki wa Manchester United Phil Jones aongeza mkataba wa miaka minne.


Phil Jones beki wa Manchester United ameongeza mkataba wake wakuendelea kubaki katika klabu ya Manchester United mkataba ambao utakwisha mwaka 2019 ikiwa ni mkataba wa miaka minne. Phil Jones ameongeza mkataba wake wakuendelea kubaki katika klabu ya Manchester United na hivyo kufanya kutokuuzwa na kwenda kwenye klabu zingine na kuweza kubaki Manchester United.


Akiongea na waandishi wa habari Phil Jones alisema kwamba anadhani kuwa klabu ya Manchester United ndiyo klabu ya pekee ya yeye kuweza kutimiza ndoto zake za mafanikio akiwa na klabu hiyo, Pia Phil Jones alisema, "Sehemu pekee yakufanya ndoto zangu zikawa kweli ni Manchester United hivyo nina kila sababu za kwenda katika klabu nyingine ila ikifika muda wa mimi kuondoka nitaondoka, Lakini Nimeamua kuongeza mkataba wangu wakuendelea kubaki Manchester United"

Naye kocha mkuu wa Manchester United, Luis Van Ghal alisema kwamba Phil Jones ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa na hivyo hatunabudi ya kumuacha aondoke ila tunachoweza kufanya nikumuongezea mkataba wa muda mrefu" hivyo ndivyo alisema Luis Van Ghal katika mkutano na wahandishi wa habari (Press Conference) wakati Phil Jones akiongeza mkataba wake.

No comments:

Post a Comment