Wednesday, June 17, 2015

Wenger: "Napenda wachezaji wanaokuwa bora wakicheza Arsenal"

Manager wa club ya Arsenal, Arsen Wenger amesema kuwa anapenda wachezaji ambao wanakujakuwa bora wakicheza katika club ya Arsenal.

Manager Wenger amesema hayo wakati akihojiwa na kituo cha runinga cha club ya Arsenal (Arsenal Tv) ambapo wakati alipoulizwa swali kuhusiana na wachezaji wanaocheza katika club hiyo. Wenger alisema kuwa yeye anapendezeshwa sana na wachezaji wanaokuja kufanya vizuri sana wakiwa katika club ya Arsenal. Wenger hakusita kutaja majina ya wachezaji ambao wamekuwa wakifanya vizuri katika club ya Arsenal ambapo alimtaja Alexis Sanchez alitokea Barcelona na kuweza kufanya vizuri sana akiwa Arsenal katika msimu uliomalizika lakini pia hakusita kumtaja Theo Walcot ambapo Wenger alisema moja kati ya wachezaji ambao anajivunia ni pamoja na Theo Walcot.

No comments:

Post a Comment