Wednesday, June 17, 2015

Airtel yazindua kampeni ya Wakati ni sasa.

Kampuni ya mawasiliano nchini, Airtel Telecommunication Company ikishirikiana na shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania, TFF, leo hii imezindua kampeni maalumu yakuibua vipaji vya soka nchini Tanzania.

TFF kushirikiana na Aritel wamezindua kampeni hiyo kwa lengo la kukuza na kuendeleza soka la Tanzania na kuifikisha Tanzania katika michuano mbalimbali inayochezwa duniani hasa katika upande wa soka. Akizungumza na wahandishi wa habari katika makao makuu ya Airtel rais wa TFF, Jamal Malinzi amesema kuwa kampeni hii ina lengo la kuifikisha Tanzania kushiriki Olympic na kombe la dunia (World Cup) kwa miaka ijayo.

Naye pia Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi. Beatrice Singano amesema kuwa kampuni ya Airtel inayonia na madhubuti ya kufikisha mbali Tanzania katika ramani ya soka duniani kwa kushiriki michuano mbalimbali. Beatrice Singano alisema pia Airtel kupitia balozi wake kwa sas ambaye ni Yaya Toure  wa Manchester City watahakikisha wanakuza vipaji na kuviendeleza.

Kampeni hiyo ambayo ilizinduliwa na mgeni rasmi kutoka wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na michezo Mkurugenzi wa wizara hiyo ambaye ni Bwana Leonard Thadeo.

Pichani:  Rais wa TFF, Jamali Malinzi, Leonard Thadeo na Beatrice Singano wakizindua kampeni ya wakati ni sasa.




No comments:

Post a Comment