Wednesday, June 17, 2015

Sergio Arguero aiokoa Argentina Copa America 2015.

Mshambulia wa Manchester City na timu ya taifa ya Argentina, Sergio Arguero jana aliipa timu yake ushindi dhidi ya mabingwa watetezi wa Copa America.

Argentina ambayo ilipata ushindi dhidi ya Uruguay kwa bao 1-0 ambapo wameweza kujihakikishia nafasi ya kubaki katika fainali za Copa America, Bao la Sergio Arguero lilifungwa katika dakika ya 56 ya kipindi cha pili na baada ya mechi kumalizika Argentina waliwezakibuka na ushindi dhidi ya Uruguay. lakini mechi nyingine ya group B ilikuwa ni kati ya Paraguay na Jamaica na timu ya taifa ya Paraguay kuweza kupata ushindi dhidi ya Jamaica.

Ushindi wa Argentina unawapeleka hadi nafasi ya kwanza katika msimamo wa group B wakifutiwa na Paraguay ambapo kwa sasa Argentina ana point nne huku Paraguay wakiwa wana point sawa na Argentina.


No comments:

Post a Comment