Tuesday, June 16, 2015

Je, Radamel Falcao atafanya vizuri akiwa Chelsea?

Mchezaji aliyesajiliwa kwa mkopo na club ya Chelsea Fc hivi karibuni akitokea Monaco ya nchini Ufaransa lakini kabla hajasijiliwa Chelsea alikuwa Manchester United ambapo pia alikuwa kwa mkopo akitokea Monaco. Radamel Falcao mwenye umri wa miaka (29) amesajili na Chelsea kwa mkopo ikiwa ni moja kati mipango ya kocha Jose Mourinho ambaye anainoa Chelsea.

Usajili wa Radamel Falcao uliweza kushtua wengi hasa waandishi wa habari na wachambuzi wa maswala ya michezo nchini Uingereza na hata dunia kwa ujumla, Usajili wa Falcao kwenda Chelsea insemekana kuwa ni moja kati ya manager  wa club ya Chelsea, Jose Mourinho ambapo Mourinho anampango wakurudisha Radamel Falcao katika kiwango chake kama kile alichokuwanacho wakati akiwa Atlectico Madrid ya nchini Spain. "Tangu Falcao asajiliwe na Monaco hakuwa katika kiwango kizuri hata baada ya kusajiliwa na Machester United kwa mkopo akitoka katika club ya Monaco pia hakuweza kufanya vizuri" alisema Manager Jose Mourinho katika gazeti la Daily Mial la Uingereza.

Radamel Falcao amesajiliwa na Chelsea ilikuziba pengo la Didier Drogba ambaye amemaliza mkataba wake na Chelsea na ameondoka katika club hiyo. Swala la usajili wa Radamel Falcao kwenda Chelsea kwa mkopo si jambo kubwa sana bali ni swala la msingi kujiuliza kwamba Je, Falcao atafanya vizuri akiwa The Blues kama aliweza kufanya vibaya akiwa Manchester United.

No comments:

Post a Comment