Sunday, June 21, 2015

Manchester United yataka kumsajili Sergio Ramos.


Manchester United ambao wapo katika harakati za kusajili wachezaji wapya ili kuweza kuapata kikosi kizuri cha kushindani na Vilabu vingine vikubwa katika michuano mbalimbali ambayo Manchester United inashiriki kwa mwaka huu wa 2015/2016.



Club ya Manchester United ikiwa katika harakati hizo za kukisuka kikosi hicho chini ya manager Luis Van Ghal ambaye ndiyo manager mkuu wa Manchester United, Club hiyo ikiwaimeshamaliza usajili wake wa kwanza wa mchezaji wa PSV na timu ya taifa ya Uholanzi Memphis Depay ambaye amesajiliwa na Manchester United hivi karibuni ikiwa huo ndio usajili wa kwanza wa Manchester United laikini bado wamekuwa wakiendelea kuwafuatilia wachezaji wengine kwa kuwataka kuwasajili ambapo wamewafuatilia wachezaji watatu wa Real Madrid ambao ni Galeth Bale, Karim Benzema na beki Raphael Varane wote wakiwa ni wachezaji wa Real Madrid.

Lakini hodi za Manchester United katika mlango wa Real Madrid hazikuishia hapo kwa wachezaji hao bali hodi zinaendelea kugongwa mlangoni mwa Real Madrid huku sasa hivi Manchester United imekuja na kishindo kikubwa cha kutaka kumsajili beki wa kati wa Real Madrid, Sergio Ramos ambaye mkataba wake unakaribia kumalizika katika club ya Real Madrid.

Manchester United wameweka nia ya kutaka kumsajili Sergio Ramos. ikiwa ni moja ya maandalizi ya kuimalisha kikosi hicho ambacho kwa mwaka huu kitashiriki michuano ya UEFA champions League pamoja na kushiriki ligi kuu ya Uingereza (EPL) michuano yote hiyo imekuwa ikiwa andaliwa na club hiyo kwa kuwasajili wachezaji kutoka timu zingine.

No comments:

Post a Comment