Sunday, June 21, 2015

Neymar Jr kufungiwa mechi nne za Copa America.


Mshambuliaji wa Brazil na club ya Barcelona, Neymar Junior da Santos mwenye umri wa miaka 23 amefungiwa mechi nne katika michuano ya Copa America baada ya kumchezea vibaya mchezaji wa timu ya Colombia wakati Brazil ikicheza mchezo wake wa pili katika hatua ya makundi na Brazil walipoteza mchezo huo kwa kufungwa 1-0 dhidi ya Colombia.
  


Neymar Jr alipewa adhabu ya kadi nyekundu kwa kumchezea vibaya mchezaji wa Colombia kwa kumpiga na mpira mchezaji huyo wa Colombia, Neymar alipewa kandi nyekundu katika mchezo huo na kutoka nje ya uwanja na kwenda kwenye vyumba vya kubadilishia nguo lakini Neymar hakwenda kwenye vyumba vya kubadilishia nguo alichokifanya alijificha kwenye kordoo ya vyumba vya kubadilishia nguo vya waamuzi na Neymar alikuwa akimsubiri mwamuzi wa mchezo.

Wakati akimsubiri mwamuzi wa mchezo wa Brazil dhidi ya Colombia, Neymar aliendelea kubaki katika kordoo ya vyumba vya waamuzi baada ya mchezo kumalizika mwamuzi wa mechi hiyo alimkuta Neymar amekaa kwenye vyumba vyao, mwamuzi alimuuliza Neymar kuwa anafanya nini katika vyumba vyao ndipo Neymar alimtolea maneno machafu na yakumkashifu mwamuzi wa mechi.

Mwamuzi aliweza kutoa ripoti ya mchezo baada ya mechi kumalizika na aliripoti pia tukio la Neymar kupewa kadi nyekundu lakini pia alitoa ripoti ya kumkuta Neymar akiwa katika vyumba vya waamuzi na tukio la Neymar kutoa maneno machafu na yakukashifu, Baada ya ripoti ya mwamuzi kupitiwa na shirikisho la mpira wa miguu la America ya Kusini liliweza kumkuta Neymar akiwa na makosa na hivyo Neymar akapewa adhabu ya kutokucheza mechi nne za Copa America lakini pia walimpa adhabu ya kulipa faini ya dola 10,000 kwa makosa aliyofanya.

Kwa adhabu zilizotolewa Neymar hatakuwepo uwanjani kwa mechi nne za michuano ya Copa America ambazo zinaendelea hii leo huku Brazil wakicheza Peru na ikiwa ni mchezo muhimu kwa Brazil kutafuta ushindi iliijihakikishie nafasi yakuingia robo fainali za Copa America.

No comments:

Post a Comment