Sunday, June 21, 2015
Lione Messi atimiza mechi 100 akiwa na timu yake ya taifa Argentina.
Mchezaji wa Fc Barcelona na timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi usiku wa jana alikuwa akitimiza mechi yake ya 100 akiwa katika kikosi cha Argentina.
Lionel Messi mwenye umri wa miaka 27 ameweza kuichezea Argentina kwa mechi 100 tangu aanze kuichezea timu yake ya Taifa ya Argentina, Usiku wa jana ambapo Argentina walikuwa wakicheza mechi yao ya mwisho katika hatua ya makundi ambapo Argentina ilichea dhidi ya Jamaica na Argentina kuweza kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Jamaica goli lilofungwa na Gonzalo Higuain.
Argentina ilipata ushindi dhidi ya Jamaica ushindi ambao unawafikisha katika hatua ya robo fainali ya Copa America, Ambapo pia mabingwa watetezi Uruguay waliweza kujihakikishia nafasi ya kuingia robo fainali baada ya kufunga Paraguay goli 1-0.
Lionel Messi ambaye ametimiza mechi 100 (Appearance) akiwa na timu ya Argentina ameweza kusaidia ushindi walioupata jana dhidi ya Jamaica licha ya kwamba hakufunga bao katika mechi hiyo. Messi ametimiza mechi hizo 100 akiwa na timu ya Argentina huku akiwa ameifungia timu ya Argentina mabao 46 tangu aanze kuichezea timu ya taifa ya Argentina.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment