Wednesday, June 24, 2015
Malinzi ampa Mart Nooij mkono wa kwaheri.
Rais wa shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF, Jamali Malinzi amempa mkono wa kwaheri alikuwa kocha wa timu ya taifa "Taifa stars" mholanzi Mart Nooij.
Akiongea na wahandishi wa habari hii leo katika hoteli ya Tansoma, Malinzi alisema kuwa TFF pamoja na kamati ya utendaji wameamua kumuaga Mart Nooij kupitia vyombo vya habari kama ilivyofanyika wakati wa utambulisho wa Mart Nooij kutangazwa kuwa kocha wa Tanzania.
Kufukuzwa Mart Nooij kunatokana na matokeo mabaya yaliyoikumba Taifa stars katika mechi zake mbili walizocheza kwa kuweza kuambulia kipigo cha mabao matatu kwa mechi zote mbili ambazo Taifa stars ilicheza ambapo katika mechi ya kwanza dhidi ya Misri ambao ulikuwa ni mchezo wa kufuzu michuano ya AFCON kwa mwaka wa 2017 ambapo Taifa stars ilipewa kipigo cha mabao 3-0 dhidi ya Misri lakini baada ya mchezo huo kumalizika Taifa stars iliweza kurejea nyumbani na kujiandaa na mechi dhidi ya Uganda ambao ulikuwa mchezo wa kufuzu michuano ya CHAN kwa wachezaji wanaocheza soka ndani ya nchi zao, Na katika mchezo huo ambao ulichezwa visiwani Zanzibar pia Taifa stars ilikubali kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya Uganda (The Cranes).
Akizungumza na wahandishi wa habari rais Jamali Malinzi alisema "Mpira wa miguu una changamoto nyingi, Watanzania bado tuna safari ndefu sana katika mafanikio yetu ya mpira wa miguu na ndio maana TFF imeanza kuwekeza katika soka la vijana sababu ndio msingi mzuri wa kuwa na timu ya taifa iliyokuwa nzuri" alisema Jamali Malinzi.
Jamali Malinzi aliendelea kwa kusema "Duniani kote chimbuko la timu bora ni soka la vijana na watoto, Tukiwa na vijana wengi walioanza kucheza mpira wakiwa katika umri mdogo watakapofikia umri wa kucheza timu ya taifa wanakuwa imara na tunapata kikosi bora cha timu ya taifa"
"Nchi za wenzetu inapofikia hatua kocha anaita kikosi cha timu ya taifa anakuwa na wigo mpana, kwetu sisi wachezaji wanaocheza soka nje ya nchi wanahesabika, Hivyo inatupasa kuwekeza katika soka la vijana." alisema rais Jamali Malinzi.
Baada ya kusema hayo rais wa TFF, Jamali Malinzi ilifika zamu ya Mart Nooij kuzungumza na wahandishi wa habari ambapo alisema. "Nawashukuru watanzania wote, serikali, wadau wa mpira wa miguu nchini Tanzania pamoja na TFF kwa sapoti walionipa nikiwa kama kocha wa timu ya taifa ya Tanzania" aliendelea kwa kusema.
"Nimefurahia sana maisha ya kuwa Tanzania kwa kipindi chote nilichokuwa nikiifundisha Tanzania, Lakini kwa kuwa imefika mwisho wa kazi yangu sina jinsi ninaamua kuondoka Lakini pia nitaendelea kuwakumbuka watanzania wote kwa sapoti yenu" alisema Mart Nooij.
TFF imeweza kumuaga rasmi hii leo kocha Mart Nooij kupitia mkutano na wahandishi wa habari ambapo rais Jamali Malinzi ameweza kumuaga Mart Nooij.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment