Friday, June 19, 2015

Sergio Aguero azungumzia tetesi za kuhama Manchester City.


Mchezaji wa Manchester City, Sergio Aguero mwenye umri wa miaka 27 aelezea kwa mara ya kwanza kuhusu uvumi wa yeye kuhamia katika club ya Real Madrid.



Aguero amesema hayo baada ya uvumi kuweza kuvuma kuhusu Sergio Aguero ana mpango wa kuhama Manchester City na kwenda katika club ya Real Madrid, akizunungumza na wahandishi wa habari (Press Conference) Aguero alisema hivi. "Sababu pekee inayonifanya kuhama club yangu ya sasa ni kutaka kushinda mataji mengi na ninaweza kushinda mataji hayo nikiwa na Manchester City"

Sergio Aguero hakuishia hapo aliendelea kwa kusema, "Siwezi kuzuia tetesi zinazoendelea na siwezi kuzuia watu kuandika wanachokiandika kuhusiana na mimi kuhama Manchester City, Lakini ninachoweza kusema ni kwamba ninayo furaha ya kuwa Manchester City. Nimepata mafanikio kwa misimu minne na nitapata mengine mengi nikiwa na Manchester City."

Bado Aguero aliendelea kusema, "Kila summer city wanaongeza wachezaji wanaotokea club mbalimbali, Hiyo ndiyo mbinu yakushinda mataji, Ninauhakika mwaka huu pia tutaongeza wachezaji wengine kwenye club ya Manchester City ili tuweze kushinda ubingwa wa ligi kuu."

Hayo ndiyo aliyosema mchezaji Sergio Aguero wa club ya Manchester City wakati akizungumza na wahandishi wa habari kuhusiana na tetesi za yeye kuhama Manchester City na kujiunga na Real Madrid.

No comments:

Post a Comment