Monday, June 22, 2015

Diego Maradona: "Nipo tayari kusimamia kiti cha uraisi wa FIFA"


Mchezaji wa timu ya taifa ya Argentina Diego Maradona amesema kwamba yupo tayari kuwa rais wa shirikisho la mpira wa miguu duniani (FIFA). Maradona ameweka nia yakutaka kuwania kiti hicho cha urais wa FIFA baada ya kutokea hari ya sitofahamu katika shirikisho la mpira wa miguu kutokea ndani shirikisho hilo, Baada ya uchaguzi mkuu kufanyika mwishoni mwa mwezi wa tano ambapo alikuwa rais wa FIFA kwa kipindi kirefu, Sepp Bratter ambaye aliweza kuibuka kidedea katika uchaguzi huo mkuu uliofanyika kuweza kumpata rais wa FIFA kwa muhura mwingine.


Baada ya Uchaguzi huo kumalizika na Sepp Bratter kuweza kuibuka kuwa mshindi wa uchaguzi huo ambapo Sepp Bratter aliweza kuwapiku wapinzani wake ambao alikuwa akishindana nao, Baada ya uchaguzi kumalizika Sepp Bratter aliweza kutangazwa kuwa mshindi wa kinyang'anyiro hicho cha kuwania kiti cha urais kwa muhura mwingine.

Sepp Bratter aliamua kung'atuka madarakani mara baada tu yakutangazwa kuwa rais wa FIFA kwa mara ya nne akiwa kama rais wa FIFA, Bratter alijiuzuru kutokana na kashfa kubwa ilyoikumba shirikisho hilo la mpira wa miguu duniani. Kashfa hiyo kubwa ya rushwa ndani  shirikisho hilo ndiyo iliyomfanya Sepp Bratter kujiuzuru nyadhifa ya uongozi wa urais wa FIFA na kuamua kuwaachia watu wengine.

FIFA ilikumbwa na kashifa hiyo kubwa ya rushwa ambapo michongo yote ya rushwa iliyokuwa ikiwaikifanyika ndani ya shirikisho hilo ilikuwa ikfanyika huku Sepp Bratter akijua dhahiri wazi juu ya michongo hiyo, Sasa baada ya kujakugundulika kuwa moja ya maofisa ambao Sepp Bratter alikuwa akifanya nao kazi moja kati yao alikuwa na wakala wa shirikisho la kijasusi (FBI) na baada tu ya kundulika kuwa ni moja kati ya maofisa ya FBI ndipo Sepp Bratter aliamua kujiuzuru na kuachia ngazi kiti cha urais cha FIFA.

Lakini baada ya Sepp Bratter kung'atuka madarakani punde tu kutangazwa kuwa rais wa FIFA kwa mara nyingine shirikisho hilo liliweza kuitisha uchaguzi mwingine wakuweza kumpata rais mwingine atakae kuja kurithi kiti kilichoachwa na Sepp Bratter, Baada ya watu wengi kujitokeza kuwania kiti hicho cha urais wa FIFA, ndipo Mchezaji wa zamani wa Argentina Diego Maradona kutangaza nia ya kugombea kiti cha Urais wa FIFA na Diego Maradona akisema kwamba yupo tayari kuwa rais wa shirikisho la mpira wa mguu duniani (FIFA).

No comments:

Post a Comment