Sunday, June 21, 2015

Baada ya kocha Mart Nooij kutimuliwa Taifa stars yapata kocha mpya wa mpito.


Kamati ya Utendaji ya shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania "TFF" imetangaza kumfukuza kazi kocha Mart Nooij pamoja na benchi zima la ufundi la Taifa stars baada ya kupata matokeo mabaya katika mechi mbili ambazo Tanzania imecheza ikiwamo mechi dhidi ya Uganda ambapo Stars ilikubali kipigo cha mabao 3-0 dhidi ya The craines ya Uganda Lakini kabla ya mechi hiyo Tanzania ilicheza mechi dhidi ya Misri katika kuwania kufuzu kombe la mataifa Afrika ambapo pia Taifa stars ilipewa kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya Misri.



Baada ya matokeo hayo mabaya yalioikumba Taifa Stars shirikisho la mpira wa miguu (TFF) kupitia Kamati ya Utendaji imemtimua kocha mkuu wa Tanzania Mart Nooij pamoja na benchi zima la Ufundi la Taifa stars. Kitu pekee cha kufanya ni kumkabidhi mikoba kocha mzawa ili aweze kuokoa jahazi la Taifa Stars.

Baada ya TFF kupitia Kamati ya Utendaji kumfukuza kazi Mart Nooij pamoja na benchi zima la ufundi hii leo TFF imemtangaza kocha mpya wa mpito wa Kuiongoza Taifa Stars ambayo ipo katika harakati ya kuwania kufuzu michuano ya AFCON kwa mwaka wa 2017 lakini pia michuano ya CHAN ambayo inahusisha wachezaji wanaocheza soka la ndani ya nchi.

TFF imemtangaza  Kocha Charles Boniface Mkwasa kuwa kocha wa mpito kwa kipindi hiki ambacho Taifa stars ipo katika hari mbaya, Mkwasa ataiongoza Taifa Stars mpaka pale atakapo patikana kocha wakujakuridhi mikoba ya Mart Nooij.

No comments:

Post a Comment