Wednesday, June 24, 2015
Liverpool imemsajili Roberto Firmino wa Brazil.
Klabu ya Liverpool imemsajili Roberto Firmino wa Brazil akitokea katika klabu ya Hoffenheim ya nchini Ujerumani kwa mkataba wa miaka mitano kwa dau la paundi milioni 29. Roberto Firmino ambaye alikuwa akigombaniwa na klabu ya Manchester United katika harakati za kutaka kumsajili mchezaji huyo wa Hoffenheim na hatimaye Liverpool imeweza kumnyaka Roberto Firmino.
Mkataba wa Roberto Firmino utaambatana na ukaguzi wa vipimo vya Afya indapo atamaliza michuano ya Copa America ambayo inaendelea huko nchini Chile huku timu ya taifa ya Brazili ikiwa imeingia katika robo fainali katika michuano ya Copa America.
Firmino ambaye ameweza kufunga mabao 47 kati ya mechi 151 ambazo Roberto Firmino amecheza akiwa na klabu ya Hoffenheim ya huko nchini Ujerumani, Roberto Firmino atakuwa ni mchezaji wa pili kuwa na thamani kubwa ya kusajiliwa na klabu ya Liverpool. Lakini Roberto Firmino hatakuwa mchezaji pekee ambaye ndiye mwenye thamani zaidi kuliko wachezaji wengine katika klabu ya Liverpool ambapo Liverpool ilishawahi kumsajili Andy Carroll ambaye alisajiliwa kwa kiasi cha paundi milioni 35 akitokea Newcastle United mwaka 2011.
Liverpool imeweza kuipiku Manchester United katika harakati za kumsajili Roberto Firmino baada ya Manchester United walitangaza kuwa walikuwa wapo tayari kumsajili mchezaji huyo kutoka katika klabu ya Hoffenheim lakini hatimaye klabu ya Liverpool imeweza kumnyakua Roberto Firmino kwa dau la paundi milioni 29 akitokea katika klabu ya Hoffenheim.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment