Muamba amesema hayo baada ya kutokea uvumi kuwa club ya Manchester United ipo mbioni kumsajili Harry Kane kutoka Tottenham. Fabric Muamba alisema hayo katika gazeti la Express ambapo Muamba alimshauri Harry Kane kutokuhiama Tottenham na kwenda Manchester United.
Harry Kane mwenye umri wa miaka 22 ambaye aliweza kufanya vizuri sana katika msimu uliomalizika kwa kuweza kushika nafasi ya pili katika orodha ya wachezaji wanaoongoza kwa magoli katika ligi ya EPL nchini Uingereza. Kane alimaliza ligi kwa idadi ya mabao zaidi ya 20 akiongozwa na mshambuliaji wa club ya Manchester City, Sergio Arguero aliyefunga mabao 23 katika msimu uliopita. Kane ambaye ameweza kufanya vizuri sana msimu uliopita hali iliofanya vilabu kadhaa vikitaka kumsajili mshambuliaji huyo wa Tottenham ambapo club ya Manchester United ikitaka kumsajili Harry Kane lakini Fabric Muamba ametoa ushauri kwa Harry Kane yakumtaka Kane aendelee kubaki katika club ya Tottenham hotspurs.
No comments:
Post a Comment