Friday, June 12, 2015

Chile yaanza vizuri katika mashindano ya Copa America 2015.

Mashindano ya bala la America ya kusini ambayo yanafahamika kama Copa America ambapo mwaka huu yanafanyika nchini Chile.

Mashindano hayo ambayo yanazihusisha timu za mataifa ya bala la America ya kusini ambapo mwenyeji wa mashindano hayo ni nchi ya Chile. timu ya Chile ambayo ipo katika group A ikiwa na timu za taifa za bala hilo ambapo ikiwemo timu ya Mexico, Ecuador na Bolivia.

Katika mchezo wa kwanza ambao ulifanyika jana tarehe 11 June ambapo wenyeji Chile walicheza na timu ya taifa ya Ecuador, mchezo huo ambao ndio ulikuwa mchezo wa kwanza wa kufungua mashindano hayo ya Copa America ambapo Chile waliweza kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ecuador na kufanya timu ya Chile kuanza vizuri mashindano hayo. timu ya Chile ambao inongozwa na wachezaji wake maarufu kama Alexis Sanchez ambaye anacheza katika club ya Arsenal na Vidal ambaye anacheza katika club ya Juventus ya nchini Italy wote hao pamoja na wengine wapo katika kikosi cha timu ya taifa ya Chile. mechi inayofuata katika group A ni kati ya Mexico dhidi ya Bolivia ambayo itachezwa leo.


No comments:

Post a Comment