Thursday, June 18, 2015

Taifa stars yatupiwa mawe na kushambuliwa na mashabiki.

Timu ya taifa ya Tanzania "Taifa stars" ilishambuliwa kwa kurushiwa mawe na mshabiki wa Taifa stars wenye uchungu na Tanzania.

Taifa stars ilishindwa kuendelea kufanya mazoezi yake baada ya wananchi kuizome na kurusha mawe kwa wachezaji wa Taifa stars amabo walikuwa wakifanya mazoezi kwaajili ya kujiandaa na michuano ya CHAN yanayowahusisha wachezaji wanaocheza soka ndani ya nchi.

Hatua ya wananchi kuizomea na kuishambulia Taifa stars inatokana na matokeo mabaya waliyoyapata katika mchezo dhidi ya Misri ambapo Tanzania ilifungwa mabao 3-0 katika mchezo huo wa kuwania kufuzu Fainali za AFCON .

Jumamosi ya wiki ijayo Taifa stars itacheza na Uganda kwenye mchezo wa awali wa kufuzu fainali za CHAN mchezo ambao utachezwa katika uwanja wa Amani visiwani Zanzibar.

No comments:

Post a Comment