Katika mchezo wa kwanza wa Argentina ambayo ilicheza na timu ya taifa ya Paraguay, katika mchezo timu ya taifa ya Argentina ndiyo ilikuwa ya kwanza kuweza kupata mabao katika mechi hiyo ambapo mabao ya Argentina yalifungwa na Lione Messi aliyefunga kwa penati na bao la pili kufungwa na Sergio Arguero kunako mwanzoni mwa kipindi cha kwanza.
Katika kipindi cha pili timu ya taifa ya Paraguay iliweza kuja na moto mkali ambao uliweza kuwapa nguvu kubwa ya kufanya mashambulizi katika lango la Argentina na kuweza kurudisha mabao yote mawili na mechi hiyo kumalizika kwa draw ya mabao 2-2.
Baada ya mechi hiyo mshambuliaji wa Argentina amesema kupitia ukurasa wake wa Facebook, kwamba walitaka kushinda mechi yao dhidi ya Paraguay lakini walitoka draw ya mabao mawili kwa mawili, Messi amewataka wachezaji wenzake wa Argentina kuweza kujituma na kucheza kama timu ya pamoja katika mchezo wao unaofuata dhidi ya Uruguay.
No comments:
Post a Comment