Friday, June 12, 2015

Azam Fc na Yanga Sports Club zaanza mazoezi kujiandaa na Kagame Cup 2015.

Club ya Azam Fc pamoja na club ya Yanga SC zimeanza mazoezi rasmi kwaajili ya kujianda na michuano ya CECAFA kwa upande wa vilabu.

Michuano ya CECAFA ambayo inhusisha vilabu vya Afrika mashariki na Kati huku timu mbalimbali za Afrika mashariki zkijiandaa na michuano hiyo.

Kwa upande wa Yanga SC ambao wao wameanza mazoezi katika uwanja wa Karume uliopo jijini Dar es Salaam wakati Azam Fc wao walianza mazoezi siku ya jumanne katika uwanja wao wa chamanzi uliopo nje kidogo na mji wa Dar es Salaam. club ya Azam pamoja na Yanga zote zimeanza mazoezi zikiwa na wachezaji wachache waliopo katika vilabu hivyo viwili vinavyo shiriki ligi kuu ya Vodacom, wachezaji ambao wapo katika vilabu hivyo ni wale ambao wamesajiliwa hivi karibuni na wale wachezaji wengine wa kimataifa wanaocheza katika club hizo mbili.





No comments:

Post a Comment